Makala
MATUMIZI YA UPANGA WA ROHO KATIKA MAOMBI YA VITA:
| Makala
MATUMIZI YA UPANGA WA ROHO KATIKA MAOMBI YA VITA:
Waefeso 6:17 "Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;"
Silaha yenye nguvu kuliko silaha zote ulimwenguni ni Neno. Neno lina nguvu kiasi Cha kuweza kuumba hata kitu ambacho hakijawahi kuwepo katika ulimwengu huu. Kwa Imani ulimwengu uliumbwa kwa Neno la Mungu. Hapa nataka nikuoneshe jinsi Neno la Mungu lilivyo na nguvu ,si kama maneno mengine uliyowahi kuyasikia au kuyasoma . Watu wengi mmekwama kwa sababu hamkuwahi kutumia Neno la Mungu vizuri ,Shetani anawaweka watu kwenye vifungo kwa kuwa hawana elimu ya Neno la Mungu au maarifa ya kiMungu.
Anasema upokeeni "upanga wa Roho"
Hii ni silaha ya Mungu mwenyewe,angalia Roho aliye andikwa hapo ni Roho mtakatifu (Roho wa Bwana) Ukisoma katika Biblia ya GNT Waefeso 6:17 " And accept salvation as a helmet, and the word of God as the sword which the Spirit gives you."
Biblia hapo juu inasema kwa lugha ya English kwamba "..the sword which the Spirit gives you." Kumbe utapokea Neno la Mungu ambalo ni Upanga kutoka kwa Roho mtakatifu. Ndiyo maana biblia ikasema katika 2 Wakorintho 10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
Silaha hizi zenye uweza katika Mungu (Maana yake Zina nguvu itokayo kwa Roho mtakatifu) Kwa maana Yeye ndiye anayekupa , Neno la Mungu pasipo uvuvio wa Roho mtakatifu halina nguvu ,maneno yote aliyokuwa anayahubiri Yesu alikuwa anayatoa kwa Roho mtakatifu
Yohana 14:10 ".. Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake."
Baba aliyekuwa ndani ya Yesu alikuwa ni Roho Mtakatifu, ndiyo maana aliwaaambia mafarisayo kwamba Yeye anatoa Pepo kwa Roho mtakatifu na si kwa belzebull mkuu wa Pepo.
Shetani huleta mbinu za kupenyeza mawazo mabaya katika Ufahamu wako yanayopingana na Neno la Mungu. Ukweli ni kwamba mawazo yana nguvu ya kujenga (yakiwa mazuri) au kubomoa hatima ya mtu (yakiwa mabovu)
Wewe ni zao la mawazo yako mwenyewe.
Hivyo ukiwa umezaliwa mara ya pili, ukweli ni kwamba Shetani anakuwa Hana kitu kwako , Wala nguvu yoyote ya kukuangamiza kwa kuwa Alisha shughulikiwa na Bwana. Hivyo Shetani hutumia mbinu ya kupenyeza mawazo yanayopinga na neno la Mungu . Mfano mzuri ni
Mwanzo 3:1 "..Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?"
Shatani anakuja na wazo la kukutoa katika kauli tii Neno la Mungu ,Kwa kuwa anaondoa utii wa Neno ndani yako kwa kukufanya uamini Yeye ni mkweli akiwa anakuonyesha uhalisia wa mzingira ya nje. Anamwambia mwanamke hautakufa hakika ,na mwanamke alivyoona matunda yanatamanika kwa macho akala na kuona yupo vilevile.
Hata hivi Leo mwovu amekuwa akiangusha kizazi hiki kwa kuwadhibitishia ukweli wa mambo yanayo onekana kwa macho ya damu na nyama kuwa ni ukweli ,na kuweka mawazo yanayopinga elimu ya Neno la kweli ya Mungu. Lakini Mungu anatuonyesha kwamba silaha tulizo nazo zinauwezo katika Roho Mtakatifu hata kuziangusha hizo ngome za mawazo ya Shetani anayopanda ndani ya fahamu zetu.
Waebrania 4:12 "Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."
Neno hili la Mungu lijae kwa wingi ndani yako katika hekima yote ,ufahamu wako ufanywe upya kwa Neno la Mungu. Hii itakufanya uwe mshindi kwa Kila wazo baya Shetani atakalotaka kulipanda ndani yako, kwa kuwa tutamshinda kwa damu ya Mwana kondoo na kwa Neno la ushuhuda wetu. Kumbuka wazo huzaa tendo na tendo huzaa tabia na tabia huzaa hatima yako. Chaguwa kuwa na wazo la Mungu kutoka katika Neno lake na kulitumia kama upanga ukatao kuwili. Amen
+255 758 708804 namba ya msaada wa kiroho kwa ushauri,maombi na maombezi.
Pastor Dr Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya ki-Mungu
SADAKA